Event Details
Photo

Posted: 2025-06-24

Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema ameridhishwa na jitihada zinazochukuliwa na Wakulima katika kilimo cha mpunga

Description

Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema ameridhishwa na jitihada zinazochukuliwa na Wakulima katika kilimo cha mpunga kwa kuongeza upatikanaji wa mpunga nchini.
\r\n \r\nAmeyasema hayo Wakati alipokua katika Ziara ya kukagua maeneo tofauti ya Kilimo katika bonde la Cheju na Mtwango Wilaya ya kati Unguja kwa kuangalia hatua zinazoendelea kwa Wakulima katika Uzalishaji wa Mpunga.

\r\n

\r\nShamata amesema Uzalishaji wa Mpunga kwa sasa umeongezeka katika bonde la Mtwango na Cheju hivyo ni vyema kuendelea kusimamia na kuzidisha mashirikiano katika kilimo chao.

\r\n

\r\nAidha Katika Ziara hiyo Shamata ameeleza kuwa ni vyema kuyaenzi mashamba hayo pamoja na kulinda miundo mbinu iliyojengwa ya vyanzo vya maji ili kuongeza Uimarishaji wa kilimo kitakachosaidia kuleta tija katika shughuli zao za kilimo.

\r\n

\r\nHata hivyo amesema kwa Upande wa Pembejeo Serikali imeongeza Upatikanaji wa mbolea kwa Wingi ili kuondosha Matatizo ya Uhitaji wa Huduma katika maeneo yote ya kilimo.

\r\n

\r\nSambamba na hayo Shamata ametoa agizo kwa wasimamizi wa mabonde hayo iwapo kuna mtu yeyote ambae hayupo tayari kulima katika maeneo hayo amesisitiza yasibaki wazi bila shughuli yoyote ya kilimo na badala yake wapewe wakulima wengine ili waweze kuendelea na kilimo.

\r\n

\r\nMapema Wakizungumza Wakulima hao walieleza kuwa wataongeza hamasa juu ya Uzalishaji wa Mpunga ili kuzuia njaa nchini na kuzingatia muda sahihi wa Kilimo ili kwenda sambamba na uvunaji wa mpunga katika maeneo yote.

\r\n

\r\nKwa Upande wake Afisa uzalishaji wa mabonde hayo wamesema kutokana na kuongezeka kwa upatikanaji wa mpunga katika mabonde hayo wameweka vikao na wakulima kwa kupanga Mipango Madhubuti ambayo imeleta tija kubwa kwao na jamii kwa ujumla.

\r\n

\r\nAmesema kwa sasa Uzalishaji wa Mpunga umeongezeka ukilinganisha na apo awali kutokana na jitihada za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za pembejeo pamoja na Wakulima kufuata miongozo kwa Wataalam wa Kilimo licha ya kua wamekabiliwa na Matatizo ya Upatikanaji wa Vifaa vya kufanyia kazi ikiwemo matrekta.

\r\n

\r\nNao Makatibu wa jumuiya ya mabonde hayo wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea mbolea ya ruzuku ambayo imeboresha uzalishaji pamoja na kuwapatia msaada wa dawa za kuulia wadudu Waharibifu wa mpunga na kuwaomba Wakulima kuacha kutumia mbolea ya chemical na badala yake watumie mbolea waliyopatiwa na Wataalamu wao.

\r\n

\r\nWaziri huyo alipata fursa ya kutembelea Eneo la maabara Ya Utafiti Wa Mifugo (ZALIRI) Ujenzi wa Ofisi ya wafanyakazi Kizimbani Pamoja na eneo linalotarajiwa kufanyika kwa maonesho nane nane dole kizimbani.

\r\n

Follow Us