- Total Visitors: 12,427
Tuesday, 21st October, 2025
Posted: 2025-10-13
Mabibi na mabwana wa mashamba kutoka Unguja na Pemba wakiwa katika ziara ya kimafunzo kwenye Shamba la Mbegu za Nafaka la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Dakawa, lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.\r\n\r\nZiara hiyo inalenga kujifunza na kuona shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na watafiti wa taasisi hiyo, ikiwemo mbinu za uzalishaji wa mbegu bora na matumizi ya teknolojia za kisasa za kilimo.\r\n\r\nZiara hiyo imeratibiwa na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar kupitia Mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula (TFSRP), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza uelewa na ujuzi wa wakulima kuhusu kilimo chenye tija na endelevu.
Fans
Followers
Followers
Subscribers