Event Details
Photo

Posted: 2025-02-19

WADAU KUTOKA WILAYA MBALIMBALI WAKUTANA PAMOJA NA WADAU WENGINE, WAMEUNGANA KUANZISHA MULTI-STAKEHOLDER PLATFORM CHINI YA MRADI WA FOLUR LENGO KUU NI KULETA MABADILIKO CHANYA.

Description

Wadau kutoka Wilaya za Kilombero na Mlimba, ZAWA, Wizara ya Ardhi, wataalamu wa misitu, pamoja na wadau wengine, wameungana kuanzisha Multi-Stakeholder Platform chini ya Mradi wa FOLUR! Lengo kuu ni kuleta mabadiliko chanya kwa maendeleo endelevu kwa kuhakikisha matumizi bora ya ardhi na maji, urejeshaji wa miti na mimea, na kuimarisha mifumo ya chakula. Kupitia ushirikiano huu, wadau wataweka mikakati thabiti ya kulinda na kuhifadhi rasilimali za asili, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, na kuimarisha uchumi wa jamii zinazotegemea ardhi na misitu. Mradi huu unatekelezwa Kaskazini Unguja kwa kuhakikisha ustawi wa mazingira na kizazi cha sasa na kijacho.

Follow Us