Posted: 2026-01-30
Afisa Kiungo wa Vijana TFSRP Zanzibar Atembelea Vikundi vya Vijana Wakulima Mkoa wa Kaskazini
Description
Afisa Kiungo wa Vijana kutoka Mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania (TFSRP) kwa upande wa Zanzibar, Sheilla Makungu Mwinyi, amefanya ziara ya kutembelea vikundi mbalimbali vya vijana vinavyojishughulisha na kilimo cha mboga mboga na matunda katika Mkoa wa Kaskazini. Ziara hiyo imelenga kubaini changamoto zinazowakabili vijana hao kama njia mojawapo ya kuwasaidia kuendeleza kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji.
\r\n

