Posted: 2025-12-08
Waziri wa Kilimo Mhe. Suleiman Masoud Makame, Azindua Zoezi la Uwekaji Bikoni Kuimarisha Mipaka ya Msitu wa Hifadhi ya Ngezi Vumawimbi.
Description
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mh. Suleiman Masoud Makame amezindua zoezi la uwekaji wa Bikoni katika mipaka ya Msitu wa Hifadhi ya Ngezi Vumawimbi, lengo likiwa ni kuainisha mipaka baina ya maeneo ya jamii na hifadhi hiyo. Uzinduzi huo umefanyika kwa madhumuni ya kulinda na kusimamia rasilimali za misitu, sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na Serikali katika uhifadhi wa mazingira. Katika hafla hiyo, Waziri aliambatana na Naibu Waziri wake, Dkt. Salum Soud Hamed, Katibu Mkuu, Saleh Mohamed Juma, pamoja na Wakurugenzi na watendaji wa Wizara hiyo kutoka Unguja na Pemba.
\r\n

