Photo

Posted: 2025-12-05

Waziri Suleiman Masoud Makame. Akutana na Uongozi wa MB Homes Kujadili Uwekezaji katika Kilimo na Mifugo Zanzibar

Description

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Suleiman Masoud Makame amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa MB Homes Huseyin Buyukballi katika ofisi za kilimo Maruhubi kujadili mwongozo wa uwekezaji katika kilimo cha maua, ndizi na miradi ya mifugo. Waziri, akiongozana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo   Saleh  Mohamed Juma na Naibu Waziri dkt Salum Soud Hamed , alieleza maeneo ya kipaumbele ya wizara na utayari wa kutoa ushirikiano wa frusa za kilimo zilizopo nchini kwa kampuni ya MB Homes na kuwataka kuanza maandalizi ya miradi hiyo kwa kufata utaratibu wa uwekezaji uliopo  kwakuwa bado mahitaji ya kuongeza  uzalishaji mazao ya chakula na biashara  za ndani na nje ya nchi zinahitajika kwa lengo la kuongeza kipato  kwa wanchi  na kukuza ajira.

\r\n