Photo

Posted: 2025-12-01

Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Salum Soud Hamed Akutana na JICA Kujadili Ushirikiano Mpya wa Miradi ya Kilimo na Mafunzo kwa Maafisa

Description

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Dkt. Salum Soud Hamed amefanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Ofisi ya JICA Tanzania  Narita Kotomi katika ofisi yake Maruhubi. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili fursa za ushirikiano kati ya wakala wa ushirikiano  wa Kimataifa wa Japan  (JICA) na Wizara yake  katika kuanzisha miradi ya pamoja ya kilimo hususan kwenye maeneo ya Umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu bora, na mazao ya matunda katika kuongeza  mnyororo wa thamani. Aidha, JICA imeonesha utayari wa kusaidia kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa Maafisa wa Kilimo ili kuwaongezea ujuzi na kuimarisha utendaji wao kwenye sekta ya kilimo. Kikao hicho kilikwenda sambamba katika kujenga msingi wa mahusiano mazuri kwa manufaa ya sekta ya kilimo nchini. Mhe. Dkt. Salum ameipongeza JICA kwa nia hiyo njema na kuahidi ushirikiano wa karibu katika kutekeleza miradi hiyo yenye tija kwa wakulima na uchumi wa taifa.

\r\n