Photo

Posted: 2025-11-29

Waziri wa Kilimo Mhe. Suleiman Makame Akagua Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Umwagiliaji, Misitu na Mifugo Kaskazini Unguja

Description

Waziri wa Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Suleiman Masoud Makame amefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kilimo cha Mpunga, Miundombinu ya Umwagiliaji, Misitu na vituo vya Mifugo. Katika Mkoa wa Kaskazini  Unguja  katika ziara hiyo, aliambatana na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Salum Soud Hamed na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saleh Mohamed Juma, pamoja na wakurugenzi na Maafisa wa wa Kilimo. Lengo la ziara hiyo ni kukagua na kuona hatua za maendeleo zilizofikiwa katika sekta hizo, pamoja na kubaini changamoto zinazokwamisha mafanikio  ya Kilimo na Ufugaji. Waziri  Suleiman aliwataka watendaji kuhakikisha juhudi za Serikali zinaendelezwa kwa kutoa huduma  kwa wakulima na wafugaji sambamba na kutunza na kuhifadhi Misitu, Wanyapori, Vyazo vya Maji  na vituo vya Mifugo vinasimamiwa kwa ufanisi ili kuongeza uzalishaji, kulinda na kuinua Uchumi wa Wananchi. Pia aliahidi kuwa serikali itaendelea kuweka mikakati bora ya kuboresha sekta hizo muhimu kwa maendeleo ya nchi  na kuwataka maafisa na wataalamu wa Kilimo kufanyakazi kwa bidii na kuwafikia wakulima kwa kuwapa utaalum itakayoleta mabadiliko ya uzalishaji.

\r\n