Photo

Posted: 2025-08-14

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuleta Mageuzi ya Kilimo Nchini.

Description

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe Hemed Suleman Abdulla wakati akifunga maonesho ya siku ya wakulima nane nane kwa mwaka 2025 yaliyofanyika kizimbani Wilaya ya Magharib \"A\"Unguja

\r\n

Amesema Sekta ya kilimo ni kiunganishi ya Sekta nyingi muhimu ikiwemo biashara,Viwanda, Utalii, na Mazingira hivyo ni dhahiri kuwa mageuzi haya yataimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji na kuimarisha masoko ya ndani.Aidha Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya Umwagiliaji katika mabonde 7 ya Mpunga Unguja na Pemba yenye ukubwa wa Hekta 20300 ili kuongeza uzalishaji wa Mpunga wenye tija ambao kwa sasa umefikia wastani wa tani 8 hadi 11 kwa hekta.

\r\n

Sambamba na hayo Serikali inakusudia kujenga vituo vya kisasa kwa kila Wilaya ambavyo vitatumika kusambasa mbinu mpya za kilimo,Mifugo naMaliasili kuanzia uzalishaji hadi sharifu wa Mazao \"Naishauri wizara ya kilimo kusimamia uzalishaji wa chakula nchini kuwa karibu na wadau ili kuleta ufanisi unaotarajiwa kuleta maendeleo ya kilimo\\\"alisema Hemed.Nae katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Umwagiliaji,Maliasil na Mifugo Ali khamis Juma alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yamehudhuriwa na washiriki 4000 wakiwa ni Tasisi za Serikali na Binafsi pamoja na wadau wa kilimo hili ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka jana.

\r\n

Ameeleza kuwa Serikali imechangiya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya uendeshaji wa maonesho ya kilimo nane nane pamoja na ujenzi wa miundombinu na majengo ya kudumu katika eneo la maonesho.Aidha amesema kwenye maonesho hayo yaliyoanza tarehe 1 mwezi wa 8 kuna vitu vingi vya kujifunza sambamba na ubunifu kutoka kwa washiriki na wadau walipo katika maonesho ambapo imekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi.Akitowa maelezo Katika ufungaji huo Waziri wa kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo amesema wizara ya kilimo ina jukumu la kusimamia upatikanaji wa mazao ya ndani na kutoa vibali ya uingizaji mazao kutoka nje ili kuwa na uhakika wa chakula kwa wananchi wake.

\r\n

Amesema ujenzi wa masoko na barabara umefanikisha ari ya kilimo nchini pamoja na upatikanaji wa frusa ya ruzuku ya pembejeo salama na rafiki kwa wakulima wote .Hivyo wakulima wanashukru kwa frusa hizi na wapo mstari wa mbele kuendeleza kilimo nchini kwa lengo la kuzalisha zaidi mazao ya chakula, matunda na mboga Mboga ambapo\\r\\nubunifu wa wakulima umefanikisha maonesho hayo kwa kiasi kikubwa.

Share This