N/AºC, Unavailable
Sunday, 31st August, 2025
Posted: 2025-07-26
Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar, Ali Khamis Juma leo tarehe 26/7/2025 amezindua kitabu cha Uzinduzi wa Mikoko huko katika Ukumbi wa Secret Garden Restaurant iliyopo Hurumzi ikiwa ni Miongoni mwa Shamra shamra za Maadhimisho ya Siku ya Mikoko Duniani.\r\n[26/07, 22:08] Salama Kilimo: Jamii imehimizwa kutunza na kulinda mazingira ya hifadhi za mikoko kwa ajili ya maisha ya sasa na vizazi vijavyo.\r\n\r\nKauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu, Said Juma Ali, alipoungana na wananchi wa Fujoni, Wilaya ya Kaskazini \"B\" Unguja, katika shughuli ya upandaji wa mikoko ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Mikoko Duniani.\r\n\r\nAkizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Said alisisitiza kuwa Zanzibar ni sehemu ya dunia, hivyo ni muhimu kusherehekea siku hii kwa pamoja kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi wa mikoko ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha ya binadamu na Viumbe wa baharini.\r\n\r\nAidha, alibainisha kuwa maeneo zaidi ya 120 ya kilimo yameathirika kwa kuingiliwa na maji ya chumvi, hali inayotokana na ukataji wa mikoko usiozingatia matumizi endelevu. Alieleza kuwa hali hiyo inatishia maisha ya wakulima na wavuvi, hivyo jamii inapaswa kuchukua hatua za haraka kulinda mikoko iliyopo.\r\n\r\nKwa upande wake Afisa mrejeshaji wa Mikoko kutoka katika Shirika la mwambao Coastal Community Network Suleiman Mohamed Salim alieleza kuwa kila mwaka katika maadhimisho ya siku ya mikoko, shirika lao huungana na Serikali kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mikoko, kuchagua aina sahihi za mikoko kwa maeneo yaliyoathirika, na kuhakikisha urejeshwaji wa mikoko katika hali yake ya asili.\r\n\r\nNaye Asha Juma Ashkina, mshiriki kutoka Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Fujoni, alisema licha ya juhudi zilizopo, bado kuna changamoto za uvamizi na ukataji wa mikoko, hali inayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.\r\n\r\nWakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Ali Khamis Juma, alizindua kitabu kipya kinachoitwa “Mangroves of Pemba”, ambacho kinaelezea aina mbalimbali za mikoko, lengo likiwa ni kuongeza uelewa na kuhamasisha utunzaji wake.
Fans
Followers
Followers
Subscribers