Event Details
Photo

Posted: 2025-12-01

Serikali Yazindua Mafunzo ya Siku 20 Kukabiliana na Wadudu na Maradhi ya Mazao Zanzibar

Description

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Suleiman Masoud Makame afunguwa Mafunzo ya utibabu wa minaza,Matunda na Mboga Mboga kwa wataalamu wa kilimo Katika chuo cha Utalii Maruhubi. Mafunzo hayo ya siku 20  yanaendeshwa na wataalamu kutoka Chuo cha Taasisi ya (CATAS )kutoka Serikali ya Watu wa China, kwa mashirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Yana lengo la kuwajengea uwezo Mabwanashamba, wataalamu na wakulima katika  kukabiliana na changamoto za wadudu na maradhi katika zao la nazi, matunda na mboga. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mhe. Suleiman alisema zao la nazi limekuwa likikumbwa na matatizo mengi ikiwemo ukataji holela, kuzeeka kwa minazi, pamoja na kukosekana kwa muamko wa kupanda minazi mipya katika mashamba, hivyo mafunzo haya ni muhimu katika kulinusuru na kulifufua zao hilo muhimu kwa uchumi na jamii ya wazanzibar.

\r\n

Follow Us