N/AºC, Unavailable
Sunday, 31st August, 2025
Posted: 2025-08-29
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Ali Khamis Juma, amewataka waajiriwa wapya wa wizara hiyo kufanya kazi kwa nidhamu, uwajibikaji na weledi ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.\r\n\r\nAkizungumza katika ukumbi wa wizara hiyo Maruhubi, Katibu Mkuu huyo aliwataka watumishi hao kutumia vyema fursa waliyoipata kwa manufaa ya taifa.\r\n\r\nSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina dhamana kubwa kwa wananchi wake. Hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo, alisema.\r\n\r\nAliongeza kuwa wananchi wanatarajia huduma bora kutoka kwa taasisi za umma, hivyo waajiriwa hao wanapaswa kuongeza nguvu kazi serikalini kwa kuonyesha ufanisi na kujituma katika majukumu yao ya kila siku.\r\n\r\nAidha, aliwasisitiza kujiepusha na makundi yasiyo na tija kazini, badala yake wajielekeze katika maeneo wanayoyapenda ili kutimiza lengo la msingi la kuajiriwa katika utumishi wa umma.\r\n\r\nKwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Noha Said Saleh, aliwataka waajiriwa hao kuheshimu viongozi, kufuata miongozo ya utumishi wa umma na kujali muda wa kufika kazini.\r\n\r\n“Heshimuni viongozi wenu, jitahidini kujenga nidhamu na uwajibikaji. Hiyo ndiyo njia pekee ya kufanikisha kazi zenu na kujijengea heshima ya kikazi,” alisema Noha.\r\n\r\nNao baadhi ya waajiriwa walieleza furaha yao na kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia ajira, huku wakiahidi kutumia nafasi hiyo kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.\r\n\r\nJumla ya waajiriwa 17 wapya wameajiriwa katika wizara hiyo na wanatarajiwa kuhudumu katika idara mbali mbali kama sehemu ya kuimarisha nguvu kazi ya utumishi wa umma ndani ya wizara na serikali kwa ujumla.
Fans
Followers
Followers
Subscribers