Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Dr. Salum Soud Hamed Akutana na Wataalamu wa China Kujadili Mradi wa JUNCAO Zanzibar
Posted: 2026-05-05

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Dr. Salum Soud Hamed Akutana na Wataalamu wa China Kujadili Mradi wa JUNCAO Zanzibar

Article Details

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhe. Dkt. Salum Soud Hamed, amekutana na kiongozi wa wataalamu kutoka China, Bw. Wang Yunyong, kujadili utekelezaji wa mradi wa JUNCAO unaolenga uzalishaji wa majani kwa ajili ya kilimo cha uyoga na malisho ya mifugo. Mradi huo, utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu katika eneo la Kizimbani, unatarajiwa kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji wadogo ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji na kipato chao. Utekelezaji wake utaongozwa na wataalamu kutoka China kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani wa wizara hiyo. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Kilimo Maruhubi na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saleh Mohamed Juma, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo, Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji Maji ambaye pia anakaimu Kilimo, pamoja na maafisa wengine wa mifugo.

\r\n