Posted: 2026-04-28
Kamati ya ZNBC Yajadili Kuimarisha Biashara ya Mazao Zanzibar
Article Details
Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Mazingira ya Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar (ZNBC), Mhe. Suleiman Masoud Makame, ameongoza kikao cha majadiliano na wajumbe wa kamati hiyo kwa lengo la kushauri na kuisaidia Baraza katika masuala yanayohusu uchumi, uwekezaji, kodi, ushindani wa kibiashara, mageuzi ya kisera pamoja na mifumo inayogusa mazingira ya biashara Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Kilimo Maruhubi na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka sekta ya umma na binafsi. Katika kikao hicho wajumbe walipata fursa ya kujadiliana kuhusu uzalishaji wa mwani, karafuu pamoja na mazao mengine, wakijikita katika mnyororo mzima wa thamani na namna ya kuendeleza biashara ya mazao yanayozalishwa Zanzibar.
\r\n

