Posted: 2026-04-27
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Ndg. Saleh Mohamed Juma Awataka Wakulima Kaskazini Unguja Kuthamini Mafunzo ya Mradi wa FOLUR.
Article Details
Katibu Mkuu Wizara Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo amewataka wakulima wa mpunga kutoka Mkoa Kaskazini Unguja kuyathamini mafunzo wanayopatiwa kwa sababu Serikali inatumia pesa nyingi. Ameyasema hayo katika Ukumbi wa skuli ya Pale iliyopa Mkoa Kaskazini Unguja wakati akifungua mafunzo ya siku nne yanayoratibiwa na mradi wa Folur. Katibu Saleh amesema mafunzo hayo yatakua hayana faida endapo wakulima hawatayatilia mkazo na kutopata matokeo mazuri iwapo hawatakifanyia kazi kile wanachofundisha. Nae Afisa Ugani wa Mradi wa Folur Salma Kombo Mshenga amesema mafunzo hayo ni endelea ya yatakua ya siku nne kwa waku hamsin (50) wa kilimo cha mpunga wa Mkoa Kaskazini Unguja kumi na 13 wakulima viongozi 37 kutoka ngazi ya jamii.
\r\n

