Posted: 2026-03-26
Wananchi wa Bumbwini Wapatiwa Mafunzo ya Ufugaji Nyuki na Uhifadhi wa Mazingira Kupitia Mradi wa Zanzibar Joint Programme
Article Details
Mafunzo yametolewa kwa wanakijiji wa Bumbwini kutoka shehia za Kiongwe Kidogo, Mafufuni na Makoba kuhusu ufugaji wa nyuki na uhifadhi wa mazingira, ikiwemo upandaji wa mikoko, kupitia Mradi Jumuishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (Zanzibar Joint Programme). Mradi huu unatekelezwa Zanzibar, ukianza na maeneo ya Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba kama maeneo lengwa. Unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kupitia Idara ya Misitu.
\r\n\r\n\\r\\n
\r\n

