Afisa Nyuki, Zainab Mmanga Ahamasisha Ufugaji Nyuki wa Kisasa kwa Uhifadhi wa Mikoko.
Posted: 2026-03-25

Afisa Nyuki, Zainab Mmanga Ahamasisha Ufugaji Nyuki wa Kisasa kwa Uhifadhi wa Mikoko.

Article Details

Afisa Nyuki kutoka Idara ya Misitu Zainab Omar Mmanga akitoa Mafunzo ya vitendo kwa Wanajamii kutoka maeneo ya Bumbwini Makoba, Kiongwe na Mafufuni Wilaya ya kaskazini  "B" Unguja.  Mafunzo hayo yalihusisha Ufugaji nyuki wa kisasa na kuzalisha Asali  yenye sifa na uhalisia. Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuimarisha uhifadhi wa Mikoko na ufugaji Nyuki wa kisasa yamefanyika Shehia ya Mwakaje na kutolewa kupitia mradi wa Pamoja Zanzibar Joint Program, yamezaminiwa na shirika la Mazingira la Kimataifa (UNEP) na kutekelezwa na ofisi ya makamu wa kwanza wa Raisi kwa mashirikiano ya Idara ya Mazingira na Idara ya Misitu

\r\n