Posted: 2026-03-23
Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Yalenga Kulinda Mikoko na Kuimarisha Mazingira Zanzibar
Article Details
Afisa Nyuki kutoka Idara ya Misitu Zanzibar, Zainab Omar Mmanga akitoa mafunzo ya Ufugaji wa nyuki kwa wanajamii wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja, yaliyofanyika katika Shehia ya Mwakaje, Wilaya ya Mjini Magharibi. Lengo la Mafunzo hayo ni kuimarisha utunzaji wa mazingira kwa kulinda misitu ya mikoko pamoja na kuendeleza ufugaji wa nyuki wa kisasa. Mafunzo hayo yametolewa kupitia Mradi wa Pamoja Zanzibar Joint Programme na kutekelezwa kwa Mashirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Idara ya Mazingira na Idara ya Misitu Zanzibar na Kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Mazingira (UNEP).
\r\n

