- Total Visitors: 130,124
Friday, 6th February, 2026
Posted: 2026-02-06
Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imefanya mazungumzo yenye lengo la kuangalia fursa za kuisaidia na kuimarisha sekta ya kilimo nchini. Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Kilimo Maruhubi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Saleh Mohamed Juma, alisema sekta ya kilimo ina miradi mingi ya kipaumbele inayohitaji kuungwa mkono. Miradi hiyo ni pamoja na uhifadhi wa misitu ya mikoko, matumizi sahihi ya madawa ya mimea na wanyama, pamoja na udhibiti wa nzi wa matunda. Alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unalenga kuongeza uzalishaji wenye tija, kukuza mazao yenye sifa za kibiashara kwa wakulima na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Kwa upande wake, Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Celine Robert, alisema shirika hilo lina dhamira ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia miradi endelevu na yenye tija. Aliongeza kuwa (AFD) inatarajia kutumia zaidi ya euro bilioni 1.5 kufadhili miradi mbalimbali kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, kama sehemu ya mchango wake katika kukuza maendeleo ya kiuchumi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
\r\nFans
Followers
Followers
Subscribers