Event Details
Photo

Posted: 2026-02-06

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhe. Suleiman Masoud Makame Aahidi Kuimarisha Ushirikiano na IAEA katika Maendeleo ya Kilimo na Mifugo

Description

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhe. Suleiman Masoud Makame, amelishukuru Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA) na kuahidi kuendelea kushirikiana, katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya kilimo na mifugo. Akizungumza baada ya kupokea ugeni  huo katika ofisi za kilimo Maruhubi,  ulioongozwa na  Gashaw Gebeyehu Wolde, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika, pamoja na Bi. Azza Kashlan, Afisa wa Usimamizi wa Programu. Waziri Makame alisema Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha ushirikiano huo unaimarika zaidi kama ambavyo umefanikiwa katika maeneo ya mazao na mifugo. Ugeni huo ulipokelewa na mwenyeji wao Profesa Najat Kassim Mohammed, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), ambaye amesema kuna haja ya kuongeza ushirikiano zaidi katika sekta ya kilimo, hususani katika tafiti zitakazotumia gharama nafuu kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo nzi wa matunda na matatizo mengine yanayoathiri uzalishaji. Kwa upande wake, Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde alisema ana matarajio makubwa ya kuona ushirikiano huo ukiimarisha usalama na uhakika wa chakula ili kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu.

\r\n

Follow Us