Posted: 2026-03-19
Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Salum Aongoza Upandaji wa Miche 250 ya Minazi Bambi
Description
Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhe. Dkt. Salum Soud Hamed, ameshiriki zoezi la upandaji wa miche 250 ya minazi katika Kituo cha Kilimo Bambi akimwakilisha Waziri Mhe. Suleiman Masoud Makame. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha uzalishaji wa zao la minazi, kuongeza kipato kwa wakulima na kukuza uchumi wa nchi.
\r\n

