Posted: 2026-03-16
Jamii Yahamasishwa Kulinda Mikoko na Kuendeleza Ufugaji wa Nyuki Kupambana na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Description
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi na Miradi kutoka Idara ya Misitu, Vuai Hassan Mkoko, akitoa mafunzo kwa wanajamii kuhusu kuimarisha utunzaji wa mazingira kwa kulinda misitu ya mikoko pamoja na kuendeleza ufugaji wa nyuki wa kisasa ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Mafunzo hayo yamefanyika katika Shehia ya Mwakaje, Mkoa wa Mjini Magharibi, yana lengo la kuimarisha uhifadhi wa mikoko na kuhamasisha ufugaji wa nyuki wa kisasa. Ambapo Jumla ya wanajamii 70 wameshiriki mafunzo hayo wakiwemo wafugaji wa nyuki, wavuvi, wasokota usumba pamoja na masheha wa shehia husika. Mafunzo hayo yametolewa kupitia mradi wa pamoja (Zanzibar Joint Programe) na kutekelezwa kwa mashirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Idara ya Mazingira na Idara ya Misitu , na kufadhiliwa na Shirika la Mataifa la Mazingira( UNEP)
\r\n

