- Total Visitors: 167,568
Saturday, 7th March, 2026
Posted: 2026-03-06
Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi imeishauri Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kuendelea kuwahamasisha wafugaji wa Zanzibar kuboresha miundombinu ya ufugaji wa kuku ili kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama ya kuku pamoja na kukuza sekta ya ufugaji nchini. Ushauri huo umetolewa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Fatma Ramadhan Mohamed, wakati wa ziara ya mafunzo katika Kampuni ya AFII Green inayojishughulisha na ufugaji wa kuku wa mayai iliyopo Kisarawe Sungwi, Tanzania Bara. Ziara hiyo ililenga kujifunza mbinu bora za ufugaji wa kisasa ambazo zinaweza kusaidia kuimarisha sekta ya mifugo, hususan ufugaji wa kuku Zanzibar. Katika ziara hiyo kamatii hiyo iliambatana na Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed, pamoja na watendaji wa wizara hiyo. Walisema lengo la ziara hiyo ni kujionea kwa vitendo namna bora ya kuendesha ufugaji wa kuku wa kisasa, jambo ambalo limewapa uzoefu mpya utakaosaidia kuwahamasisha wananchi, hususan wanawake na vijana, kujikita katika shughuli za ufugaji. Hata hivyo walisema wameridhishwa na namna shughuli za ufugaji zinavyoendeshwa katika kampuni hiyo na kueleza kuwa uzoefu walioupata utasaidia kuhamasisha makundi ya wanawake pamoja na vijana kuingia katika sekta hiyo ili kujipatia ajira na kipato.
\r\n\r\n\\r\\n\\r\\n
\r\n\r\n"Kwa kweli tumevutiwa sana na ziara hii. tumejionea shughuli za ufugaji wa kuku zinazofanyika kwa ubora mkubwa tofauti na maeneo mengine tunayotembelea, Hivyo tutachukua jukumu la kuwahamasisha makundi ya wanawake na vijana kujikita katika ufugaji kwani una uwezo mkubwa wa kutoa ajira na kipato cha kuendesha maisha,” kamati ilisema. Walongeza kuwa vijana wengi wamekuwa wakikimbilia sekta ya utalii pekee kutafuta ajira, huku sekta ya ufugaji ikiwa na fursa kubwa ya kuwapatia kipato na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.
\r\n\\r\\nAidha, wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia uwezekano wa kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mikopo nafuu ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi ya ufugaji wa kuku, jambo ambalo pia litasaidia kufungua ajira kwa vijana wengine. Hata hivyo, kamati hiyo ilisisitiza umuhimu wa kuweka miundombinu bora ya ufugaji kwa wafugaji wa kuku Zanzibar ili kuongeza tija katika uzalishaji. Sambamba na hayo walibainisha kua matumizi ya vifaa bora vya ujenzi wa mabanda ya kuku, ikiwemo matumizi ya plastiki maalumu kwa ajili ya kuezekea, yanaweza kusaidia kupunguza joto kali na kuruhusu hewa safi kuingia ndani ya mabanda, tofauti na mabati ambayo mara nyingi husababisha joto kali linaloweza kuathiri afya na ukuaji wa kuku. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed, alisema ziara hiyo imewapa fursa muhimu ya kujifunza kuhusu mifumo ya kisasa ya uzalishaji wa kuku wa mayai inayotekelezwa na mwekezaji huyo. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo na mifugo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza ajira kwa wananchi. Dkt. Salum ameeleza kuwa baada ya ziara hiyo, wajumbe wa kamati pamoja na watendaji wa wizara watakaa pamoja kutathmini mambo waliyojifunza na kuona namna bora ya kuishauri Serikali ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika ufugaji wa kuku wa kisasa Zanzibar. Alifafanua kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar katika sekta ya mifugo, jambo litakalosaidia kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kutoa elimu ya kisasa ya ufugaji kwa wafugaji wa ndani. Aidha, alisema wafugaji wa Zanzibar wanatarajia kuona mabadiliko makubwa katika sekta hiyo kutokana na mpango mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo na mifugo, ikiwemo kuongeza uzalishaji wa kuku na kuanzishwa kwa taasisi au chuo kitakachotoa mafunzo ya ufugaji wa kisasa. Sambamba na hayo, Dkt. Salum amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa juhudi zake za kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, mifugo na umwagiliaji, hatua ambayo inaendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi. Mapema akizungumza, mwekezaji wa kampuni hiyo Mao Xiaojiang, ameushukuru ujio wa ujumbe huo akisema umeimarisha mahusiano na kubadilishana uzoefu katika sekta ya ufugaji. Alisema wageni hao wamepata fursa ya kujionea namna ufugaji wa kisasa unavyofanyika kuanzia utunzaji wa vifaranga hadi kufikia hatua ya uzalishaji kwa kuzingatia viwango vya ubora. Aliongeza kuwa ziara hiyo ya kimafunzo kati ya Zanzibar na Tanzania Bara itaendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ufugaji na kusaidia kubadilishana teknolojia za kisasa za uzalishaji. Kampuni ya AFII Green imeajiri jumla ya wafanyakazi 65, wengi wao wakiwa vijana wazawa wa eneo hilo, na huzalisha takribani vifaranga laki sita kila mwezi.
\\r\\n
\r\nFans
Followers
Followers
Subscribers