- Total Visitors: 155,959
Thursday, 26th February, 2026
Posted: 2026-02-25
Kikao cha Kamati Uongozi cha Mradi wa Mifumo ya Chakula, Matumizi ya Ardhi,maji na Urejeshaji wa Mandhari ya Misitu (FOLUR) kimefanyika kwa lengo la kuimarisha usimamizi na uangalizi wa mradi pamoja na utekelezaji wa Mpango Kazi na Bajeti ya mwaka 2025/2026 na kuangalia bajeti mpya. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Saleh Mohamed Juma, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Bara, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Ramada Hotel, uliopo Mbezi Beach Resort.
\r\nFans
Followers
Followers
Subscribers