- Total Visitors: 126,749
Wednesday, 4th February, 2026
Posted: 2026-02-02
Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Mohamed Dhamir Kombo, wakishirikiana na watendaji wa Wizara, wamepokea ugeni kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Joel Laurent ambapo
\r\nUgeni huo umefika Wizara ya Kilimo Zanzibar kwa ajili ya kufanya mazungumzo yenye lengo la kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kuhusu matumizi sahihi ya mbolea, usajili, ukaguzi wa mbolea bora pamoja na kuimarisha uhamasishaji kwa wakulima.
\r\nHatua hiyo inalenga kuboresha usimamizi na uratibu wa matumizi ya mbolea ili kuongeza tija na kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kupitia sekta ya kilimo Zanzibar
Fans
Followers
Followers
Subscribers