- Total Visitors: 85,040
Thursday, 1st January, 2026
Posted: 2025-12-18
Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Suleiman Masoud Makame amesema wataendelea kuwashajihisha na kuwaunga mkono wafugaji wa kuku ili kuongeza hamasa ya kuongeza ufugaji wa kuku katika jamii
\r\n\r\nAmeyasema hayo wakati wa ziara ya kuwatembelea wafugaji wa kuku katika maeneo tofauti Wilaya ya Kaskazini na Wilaya ya kati Unguja ameeleza kuwa kwa wafugaji ambao wanauelewa mkubwa katika shughuli ya ufugaji ni vyema wakashirikiana na wafugaji ambao wanauhaba wa elimu ya ufugaji ili waweze kuzalisha kitaalamu na kufikia lengo
\r\n\r\n
\r\nAmesema uongezekaji wa ufugaji wa kisasa nchini ni adhma ya Serikali kupitia Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi ya kuongeza upatikanaji wa chakula cha uhakika kwa Zanzibar na kuacha ufugaji wa kimazowea na kufuga ufugaji wa kisasa ili kuinua pato la Taifa sambamba na upatikanaji wa ajira kwa wananchi
Aidha kwa upande wa Naibu Waziri wa kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Dr. Salum Soud Hamed amesema kuna muelekeo wa ufugaji mzuri wa ufugaji wa kisasa na kibiashara na wenye tija kwa kushirikiana na Bank ya Maendeleo ya kilimo (TADB) ambao wamekuwa wadau wakubwa wa Maendeleo katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia mikopo wafugaji sambamba na utowaji wa elimu ili kufuga kwa kupata faida
\r\n\r\nAmesema lengo la Bank hiyo ni kuona wafugaji wanapata maendeleo na kujitatua kiuchumi ameeleza kuwa kwa upande wa Wizara ya Kilimo ni faraja kuwa na wadau wanawaunga mkono wafugaji na kuwaona wafugaji wanasimamia vyema fursa zilizopo
\r\n\r\n
\r\nAidha kwa upande mwengine amewataka wafugaji wengine ambao bado hawajaingia katika ufugaji wa kisasa na wenye tija wafike katika idara ya Maendeleo ya Mifugo kupatiwa maelekezo ili na wao waweze kufuga ufugaji wa kisasa ili kufikia dhamira ya Serikali kuwainua wananchi kiuchumi na kufikia malengo waliojiwekea
Kwa upande mwengine ameeleza kuwa ufugaji wa kuku utaweza kuwapatia ajira na kupata usalama wa chakula nchini amesema upo uhitaji wa kuku jambo ambalo litapelekea upatikanaji wa fursa za soko ya uhakika wa bidhaa zitokanazo wa uzalishaji wa kuku hao
\r\nAidha kufuata utaratibu wa ufugaji ili kufuga kiusalama na kuweza kuzalisha mayai yenye ubora na siha kwa watumiaji na kupata masoko ya kitaifa na yakitali .
\r\nKwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar Asha Zahran Mohammed amesema mkakati wa Idara ni kuwafikia wafugaji wote kuwapatia elimu ili waondokane na ufigaji wa kimazowea na kufuga ufugaji wa kibiashara ili kuongeza udhalishaji kwa wingi na kufikia ufugaji wa kibiashara
Amesema matarajio yapo makubwa ya kuongezeka kwa udhalishaji wa ndani wa mayai kutokana na kuwepo kwa wafugaji wanaozalisha kwa siku trea 250 za mayai na kuongeza zaidi ya kiwango hicho kwa siku ili tuweze kujitosheleza nchini na kuacha uagizishaji wa mayai kutoka nje ya Zanzibar
\r\n\r\nAmesema kwa ya Idara ya Maendeleo ya Mifugo ina takwimu zinaonesha uzalishaji wa kuku wa yai kwa hapa Zanzibar umefikia asilimia 70 ukilinganisha na apo awali kwa kushirikiana na bank ya maendeleo kilimo kwa kutoa mikopo kwa wafugaji wa kuku wa yai
\r\n\r\nKwa upande wa Afisa biashara kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Abio Ntakisigaye amesema wanafaraja kutokana na ziara hiyo itapelekea kuongeza juhudi za wafugaji na kuongeza uzalishaji na kuweza kusaidiwa na Serikali .
\r\n\r\nAmesema Bank ya maendeleo ya kilimo haipo katika utowaji mikopo inajishuhulisha na utowaji wa elimu ili kuhakikisha wanaweza kutatua matatizo yanayojitokeza kwenye miradi yanaweza kutafutiwa ufumbuzi na kuweza kupata maenedeleo mazuri katika jamii.
\r\nFans
Followers
Followers
Subscribers