Event Details
Photo

Posted: 2025-11-25

Kikao cha makatibu wakuu na wakurugenzi watendaji kimefanyika katika Hoteli ya Verde

Description

Kikao cha makatibu wakuu na wakurugenzi watendaji kimefanyika katika Hoteli ya Verde, Maruhubi Zanzibar, kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Saleh Mohamed Juma . Kikao kilijadili utekelezaji wa Mradi wa Mageuzi ya Ufugaji wa Maziwa unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi, unaofadhiliwa na  IFAD Mashirika Binafsi  na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mradi  huo wenye lengo la kuboresha Sekta ya ufugaji wa ng’ombe  wa maziwa kwa njia rafiki  kwa Mazingira,kuongeza uzalishaji  ili kuinua kipato na lishe. Washiriki walisisitiza ushirikiano na ufuatiliaji madhubuti kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa mafanikio Tanzania Bara na Zanzibar.

\r\n

Follow Us