REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

MINISTRY OF AGRICULTURE, IRRIGATION, NATURAL RESOURCES AND LIVESTOCK

NEWS AND EVENTS


60% Complete (warning)
  • 2023-05-11
  • MKOA WA KUSINI UNGUJA WAPANDA MITI KATIKA MSITU WA HIFADHI WA JAMBIANI MUYUNI

    Jumla ya miti asili elfu mbili imepandwa katika eneo la hifadhi ya jambiani muyuni katika eneo lililoathirika na moto lenye ukubwa wa takribani hekta mia moja ili kurejesha uoto wa asili uliopotea. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Rajab Yussuf Mkasaba Afisa misitu wa wilaya hiyo Idrisa Hamdani idrissa amesema hatua hiyo itasaidia kurejesha uhalisia uliopotea katika eneo hilo. Amesema msitu wa hifadhi ya jambiani unafaida kubwa hivyo amewataka wakulima kuacha

    Read More
  • 2023-05-08
  • WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MHE. SHAMATA SH. KHAMIS ASEMA AMANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO

    Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo imesema Amani katika nchi ndio msingi wa maendeleo wa kua endelevu katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo hususan kwa Upande wa Bara la Afrika Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Shamata shaame khamis aliyasema hayo huko Katika Ukumbi wa Wizara hiyo Maruhubi wakati alipokua akifungua kikao cha majadiliano cha washiriki wa kozi kutoka katika chuo cha Taifa cha Ulinzi wakiwemo na washiriki kutoka katika nchi mbali mbali barani

    Read More
  • 2023-04-20
  • WAZIRI SHAMATA AWATAKA WATAALAMU WA TAASISI YA ZARI NA ZALIRI KUJENGA MASHIRIKIANO

    Wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zanzibar (ZARI) na Taasisi ya Utafiti wa mifugo Zanzibar (ZALIRI) wametakiwa kujenga mashirikiano ya pamoja katika kutoa mashirikiano mazuri ya matokeo ya utafiti ili yaweze kuwafikia walegwa kwa wakati Waziri wa kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis ametoa rai hiyo huko katika Ukumbi wa maabara ya mazao Kizimbani wilaya ya Magharibi A unguja wakati alipokua katika kikao cha bodi ya wakurugenzi ya ZALIRI kilichojadili

    Read More
  • 2023-04-13
  • ZARI YAFANYA UTAFITI WA MBEGU YA MUHOGO ILI KUKABILIANA NA ATHARI YA MARADHI YA MICHIRIZI YA KAHAWIA

    Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar ZARI kwa kushirikiana na Taasisi ya kimataifa ya Mazao ya Joto imefanya Tafiti za Tathmini mbegu bora za muhogo ili kukabiliana na athari za maradhi ya michirizi ya kahawia ya muhogo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar Dkt. Mohamed Dhamir Kombo ameeleza hayo huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi A Unguja alipokua akizungumza na watafiti, mabwana shamba na wakulima wakati wa uvunaji wa zao la muhogo uliopatikana katika utafiti

    Read More
  • 2023-03-15
  • WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI MICHE YA MIKARAFUU

    Waziri wa Kilimo, Umwagilaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis akiwa katika uzinduzi wa ugawaji wa miche ya mikarafu kwa msimu huu alisema karafuu ni zao linaloimarisha uchumi wa zanzibar kwa kuwa ni zao la biashara linalo vitangaza viziwa vya unguja na pemba duniani kote pamoja na kuingizia serekali mapato.


    Amesema Serekali kwa kutambua na kuona thamani ya zao la karafuu inaendelea kufanya juhudi za kupandisha bei ya karafuu,kuwapa vifaa na mikopo pamoja na

    Read More
  • 2023-02-27
  • KATIBU MKUU AKABITHI TANI 88 ZA MBEGU YA MPUNGA

    Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Ndg: Seif Shaaban Mwinyi amekabidhi tani 88 za mbegu za mpunga aina ya Saro 5, TXD 88 na SuPa PADDY yenye gharama ya shiling za kitanzania 227,000,000 kwa jumuiya ya wa wakulima wa bonde la Cheju ambayo itauzwa kwa wakulima kwa bei ya shiling 1300 kwa kilo moja. Amesema hayo huko chenju alipokuwa akikabidhi mbegu hiyo kwa Jumuiya ya Wakulima ya bonde la Cheju


    Amesema fedha za ununuzi wa mbegu hizo zimetolewa

    Read More
  • 2023-01-30
  • KATIBU MKUU AKUTANA NA MAKAMO WA RAIS KUTOKA KAMPUNI YA KISERIKALI YA KOREA

    Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili Na Mifugo Seif Shaaban Mwinyi Amesema Ujio Wa Makamo Wa Rais Kutoka Kampuni Ya Kiserikali Ya Korea Kusini KRC itazidi kuimarisha mashirikiano makubwa katika sekta ya kilimo kati ya Zanzibar na nchi yao katika kuendeleza miradi ya Umwagiliaji Maji unaondelea sasa na itakayoanza baadae. Amesema kuwa lengo la ujio huo ni kuangalia ufanisi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji ambapo awamu ya kwanza umekamilika kwa asilimia 100 kwa

    Read More
  • 2023-01-06
  • SEKTA YA UTALII ITAIMARIKA IKIWA WAGENI WATAKUWA NA IMANI KUWA ZANZIBAR WATAPATA CHAKULA SALAMA AMBACHO HAKINA MADHARA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uwezeshaji, Wananchi Kiuchumi Mhe: Mudrik Ramadhani Soraga amesema Sekta ya utalii itaimarika ikiwa wageni watakuwa na Imani kuwa Zanzibar watapata chakula salama ambacho hakina madhara. Alisema serikali kwa kutambua suala hilo imeimarisha miundonbinu ya kuhifadhia chakula kwa kulinda usalama wa wageni Kuimarisha sekta ya utalii nchini

    Alisema suala la kudhibiti Sumu kuvu ni muhimu ndio maana serikali kupitia Wizara ya Kilimo Umwagiliaji

    Read More
  • 2023-01-04
  • MAKAMO WA KWANZA WA RAIS MH. OTHMAN MASOUD OTHMAN AMESEMA KILA MMOJA ANAWAJIBU WA KULINDA NA KUTUNZA HIFADHI HAI YA JOZANI GHUBA YA CHWAKA

    Makamo wa Kwanza Wa Rais Mh. Othman Masoud Othman amesema kila mmoja anawajibu wa kulinda na kutunza hifadhi hai ya jozani ghuba ya chwaka ili kusaidia kubaki salama na kuwa kivutio kikubwa cha wageni Akizindua hifadhi hiyo huko jozani wilaya ya kati Mh Masoud amesema hatua hiyo itasaidia hifadhi hiyo kutoathiriwa na wananchi ambao hawana uwelewa kuhusu hifadhi hai

    Amesema kumekua na matatizo mengi katika hifadhi hai kwani wapo watu hutumia hifadhi hiyo kwa kukata miti,

    Read More
  • 2022-12-14
  • KATIBU MKUU AMETIA SAINI MAKUBALIANO YA UHIFADHI WA MSITU WA JAMBIANI MUYUNI NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ROORS & SHOOTS FREDERICK KIMARO

    KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO UMWANGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO SEIF SHAABAN MWINYI AMETIA SAINI MAKUBALIANO YA UHIFADHI WA MSITU WA JAMBIANI MUYUNI NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ROORS & SHOOTS FREDERICK KIMARO KUTOKA TANZANIA YALIYOFANYIKA KATIKA OFISI ZA KILIMO MARUHUBI AMESEMA LENGO LA SEREKALI KUFIKIA HATUA ZA MAKUBALIANO YA KUUHIFADHI MSITU WA JAMBIANI MUYUNI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA AMBACHO KITAWEZESHA KUWA NA FAIDA KWA NCHI NA JAMII KWA UJUMLA AIDHA AMEELEZA KUWEPO KWA MISITU YA

    Read More
  • 2022-08-10
  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE: DR. HUSSEIN ALI MWINYI AHIMIZA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUITUMIA FURSA YA MAONESHO YA NANE NANE KUTAFUTA ELIMU SAHIHI YA MATUMIZI YA ZANA ZA KISASA.

    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wakulima na wafugaji wanaoshiriki maonesho ya Nane nane kuitumia vyema fursa hiyo kutafuta elimu ya matumizi sahihi ya zana za kisasa, mbegu bora na pembejeo ili kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuleta Mapinduzi ya Kilimo na Ufugaji nchini.

    Dk. Mwinyi ametoa wito huo katika Ufunguzi wa Maonesho ya kilimo Nane nane yaliofanyika Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

    Amesema wakulima na

    Read More
  • 2022-07-04
  • WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MH: SHAMATA SHAAME KHAMIS AMEZINDUA KAMPENI ZA KUDHIBITI NZI WA MATUNDA

    Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis amezindua Mradi wa kampeni ya kudhibiti nzi wa matunda uliyofanyika Kitope Zanzibar. Amesema Zanzibar ina fursa kubwa ya uzalishaji wa matunda na mboga, ambayo ni chanzo cha upatikanaji wa kipato Kwa wakulima wadogo wadogo, hata hivyo uvamizi wa nzi wa matunda umekua changamoto kwa uzalishaji na ubora wa mazao Kama vile embe, mapapai na mabungo. Nzi waharibifu wa matunda ambao wamejitokeza Zanzibar mnamo mwaka

    Read More
  • 2022-06-25
  • WAZIRI WA KILIMO MHE. SHAMATA AKABIDHI BASKELI KWA VIONGOZI WA VIKUNDI VYA KUKOPA NA KUWEKA

    Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe Shamata Shaame Khamis amekabidhi baskeli 30 pamoja na visanduki 30 kwa baadhi ya viongozi wa vikundi vya kuweka na kukopa kutoka Shehia mbali mbali vinavyojishuhulisha na kilimo na ufugaji. Vitendea kazi hivyo vimetolewa kupitia mradi wa viungo uliochini ya usimamizi wa Agri-Connect vyenye thamani ya shilingi milioni Saba na laki tano 7,500,000. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili

    Read More
  • 2022-06-08
  • UZINDUZI WA LISHE ZANZIBAR

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo pamoja na Shirika la Chakula Duniani (FAO) kwa ufadhili wa Nchi za Ulaya (EU), wamezindua kampeni ya Lishe bora Zanzibar ambayo ilifanyiaka katika viwanja vya bustani ya Forodhani Zanzibar saa 10 jioni tarehe 29/05/2022.

    Kampeni hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis, alisema muongozo wa chakula utawezesha Serikali

    Read More
  • 2022-05-17
  • WAZIRI WA KILIMO, UMWAGILIAJI, MALIASILI NA MIFUGO AKUTANA NA WADAU WA KILIMO HAI - MILELE FOUNDATION

    Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis amekutana na wadau wa kilimo hai Milele Foundation katika kujadiliana juu ya kuendeleza pamoja na kumaliza mpango kazi wa kilimo hai hapa Zanzibar.

    Aidha, Mheshimiwa Shamata aliwataka Milele Foundation kuendeleza mpango kazi huo ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na kuwa tegemezi wa wananchi wa Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za Milele Foundation huko Mweni nje kidogo na Mji wa

    Read More