UTANGULIZI
Idara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula ni moja kati ya Idara kongwe katika Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo.
MAJUKUMU MAKUU YA IDARA
Lengo kuu la Idara ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kuchangia pato la nchi, mapato ya wakulima na kupunguza utegemezi wa kuagiza mazao ya chakula kutoka nje ya Zanzibar.
Kwa kusimamia utekelezaaji wa lengo hilo kuu Idara ina majukumu yafuatayo:
- Kuratibu upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima wa Zanzibar.
- Kusimamia kazi za Utibabu wa mimea na ukaguzi wa mazao, ikiwemo upatikanaji wa dawa za wadudu na magugu, na mitego ya kunasia nzi wa matunda.
- Kufuatilia kazi za utoaji wa elimu kwa wakulima pamoja na utoaji wa ushauri wa kitaalam, kazi hizi zinafanyika kupitia divisheni ya Elimu kwa Wakulima, kwa kushirikana na Manispaa na Halmashauri za Wilaya.
- Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za mazao yote kwa Unguja na Pemba. Takwimu hizi ni pamoja na ukubwa wa maeneo yanayolimwa vipando mbali mbali, mazao yanayozalishwa mashambani na yale yanayoletwa Sokoni.
- Kutayarisha ripoti za robo mwaka kwa mfumo wa Bangokitita, kutayarisha Bajeti ya mwaka ya Idara na ripoti nyingine zitazotakiwa na Wizara.
- Kuunda kamati tendaji ya Idara ambayo inakusanya wakuu wa Divisheni, Maofisa Kilimo wa Mikoa na Wilaya na Wakuu wa vituo vya Kilimo. Kamati hii ni kwajili ya kumsaidia Mkurugenzi kwa mashauri mbali mbali kupitia vikao vyake.