
KATIBU ALI KHAMIS ASEMA USHIRIKISHWAJI WA JAMII NI NJIA PEKEE YA USIMAMIZI WA MISITUPosted: 2024-04-09
Katibu Mkuu Wizara ya kilimo,Umwangiliaji,Maliasili na Mifugo Ndg: Ali Khamis Juma
Amesema ushirikiswaji wa jamii katika kutoa maoni yao ndio njia pekee itakayo saidia usimamizi mzuri wa misitu ya hifadhi.
Akizungumza katika kikao cha mpango kazi wa usimamizi wa Msitu wa akiba wa Kidikotundu, Nongwe na Vundwe kilichowashirikisha wa wadau kutoka tasisi za Serekali na binafsi,wasimamizi wa misitu,wanyama pori na wanajamii kutoka Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema lengo la kuwasilisha Mpango wa usimamizi wa msitu wa kidikotundu kwa wadau ni kuwa na Muongozo utakao tumika katika uendeshaji wa shughuli zote za hifadhi Mpya ya misitu huo.
Aidha aliwataka wadau na wanajamii kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni juu ya mpango huo kutokana na umuhimu wa uwepo wa misitu na madhara yatakayotokea tukikosa misitu kwa maisha ya wanadamu na wanyama.
Mratibu wa Jumuiya ya uhifadhi wa wanyamapori Tanzania Said Abdallah Faki Amesema adhima ya kuelekeza harakati za uhifadhi misitu imetokana na matokeo ya utafiti kuonesha kwa asilimia 30 ya miti na wanyama adimu hupatikana katika msitu wa Kidikotundu ambayo ndio rasilimali ya nchi na husaidia jamii kupata kipato chao
Akitoa maoni yake kwenye kikao hicho mwanajamii wa Misitu wa hifadhi Muyuni Ismail Suleiman amesema matarajio ni kuwa na mafanikio kwa jamii na kupata maendeleo katika miradi mbali mbali ya uhifadhi