
Ni Jukumu la Viongozi katika Sekta ya Kilimo kufanya ziara kwenye maeneo ya wakulima Posted: 2023-06-19
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Seif Shaaban Mwinyi, amesema ni jukumu la viongozi katika sekta ya kilimo kufanya ziara kwenye maeneo ya wakulima ili kujua changamoto na mafanikio yanawakabili Akizungumza huko Mtwango wilaya ya Magharibi alipofanya ziara ya kuzitembelea Jumuiya za wakulima kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika bonde hilo. Alisema dhamira ya ziara hiyo ni kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha mpunga katika msimu wa masika ambao umeweza kupiga hatua nzuri.
Seif ameeleza kuwa maandilizi ya upandaji wa mpunga huo yameleta ufanisi unaowapa faraja viongozi wa wizara hiyo kutokana na mavuno makubwa wanayotarajia kupatikana. Amesema juhudi zinaizochukuliwa na wakulima wa jumuiya hiyo zilizoweza kuwa na matunda mazuri katika kilimo chao kwani anaamini kutokana na jitihada hizo walizozichukua zinazotarajia kupunguza uagiziaji wa mchele. Alieleza kuwa hali hiyo itaongeza kwa kias kikubwa kwa mapato ya wakulima na wafanyabiashara na wakulima kwa kipindi cha mwaka mzima Akizungumzia suala la upatikanaji wa mbolea, Katibu huyo amesema kuwa kwa sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinafanya jitihada za kutatua changamoto hiyo kupitia ruzuku ya pembejeo ili liweze kutatuliwa kwa wakati muafaka. .
Akizungumza na wakulima hao, Mkurugenzi Idara ya Umwagiliaji maji, Haji Hamid Saleh, amesema kutokana na juhudi za serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuwapatia mafunzo ya kilimo cha mpunga wakulima. Haji aliongeza kwa mafunzo hayo yaliwaongoza kufikia malengo waliyokusudia ya kuongeza uzalishaji.
Nae Mwenyekiti wa jumuiya ya wakulima wa bonde hilo, Justas Assac Aton, amesema katika bonde hilo wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vitendea kazi na kuiomba wizara kuwapatia vifaa muhimu vya kilimo endelevu wazidi kulima kwa wakati na kuimarisha kilimo chao. Bonde la Mtwango ni miongoni mwa bonde la Umwagiliaji ambapo lina ukubwa wa hekta 83.6 na lina wingi wa wakulima ikiwemo wanawake na wanaume 598.