
KATIBU MKUU AKUTANA NA MAKAMO WA RAIS KUTOKA KAMPUNI YA KISERIKALI YA KOREAPosted: 2023-01-30
Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili Na Mifugo Seif Shaaban Mwinyi Amesema Ujio Wa Makamo Wa Rais Kutoka Kampuni Ya Kiserikali Ya Korea Kusini KRC itazidi kuimarisha mashirikiano makubwa katika sekta ya kilimo kati ya Zanzibar na nchi yao katika kuendeleza miradi ya Umwagiliaji Maji unaondelea sasa na itakayoanza baadae. Amesema kuwa lengo la ujio huo ni kuangalia ufanisi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji ambapo awamu ya kwanza umekamilika kwa asilimia 100 kwa mabonde matatu nayo ni Kinyasini, Mlemele na Cheju na mabonde mengine yanaendelea kutatuliwa changamoto zilizojitokeza. Kwa sasa wamekuja kwa kuanza matayarisho ya mradi katika awamu ya pili ambao mkopo wa dola za Kimarekani 18.1 utasainiwa hivi karibuni baina ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Exim Bank ya Korea.
Sambamba na hilo pia ameeleza mradi ambao unalengo la kusaidia mafunzo kwa wakulima na vifaa vya ukulima kama ni mradi wa msaada kutoka Serikali ya Korea. Katibu Mkuu amefahamisha kuwa uendelezwaji wa mradi huo wa Umwagiliaji maji utasaidia Zanzibar kupiga hatua ya Uzalishaji wa Mpunga na kuweza kufikia hatua ya kujitosheleza kwa Chakula na kupunguza kuagiza mchele kutoka nchi za nje.
Makamo wa Rais wa Korea Kang, Kyung-hag amesema amefurahishwa na ushirikiano wa Zanzibar kwa kuwa pamoja hususan katika sekta ya kilimo na kuweza kutoa fursa kwa wakulima kulima kilimo cha kisasa sambamba na kutoa elimu kwa wataalamu na kutoa uzoefu kwa wataalamu na kujenga mashirikiano yao ya pamoja Mradi huo miundombinu ya Umwagiliaji utaanza utekelezaji wake rasmi July 2024 ambapo jumla ya dola za kimarekani milioni 5.5 ni msaada kutoka Serikali ya korea.