MINISTRY OF AGRICULTURE, IRRIGATION,
NATURAL RESOURCES AND LIVESTOCK (MAINRL)

Nzi waharibifu wa matunda

Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na  biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya  waharibifu  wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda  na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda. ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA. Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ya jamii hizo ni jamii sita zinazofanya uharibifu wa matunda na mboga mboga. Katika jamii hizi kuna aina mbali mbali za nzi wagharibifu. Hata hivyo kila jamii ina asili ya eneo au maeneo Fulani ya Kijografi . Jamii zenye asili ya bara la Afrika ni Dacus na Ceratitis . Zipo baadhi ya aina za Nzi wagharibifu wa matunda ambazo zimevamia maeneo mengine kwa mfano Nzi wa Mediterenian (Ceratitis Capitata) ni Nzi mwenye asili ya Afrika , lakini kwa sasa amesambaa karibu ulimwengu wote, vile vile Nzi mvamizi (Bactocera Invadens ) mwenye asili ya Bara la Asia amevamia Bara la Africa mwaka 2003. Nzi wagharibifu wa Matunda ni tofauti na wale Nzi wadogo wanaojulikana kwa jina la Drosophila ambao huonekana kwenye matunda na vyakula vilivyooza.
Katika Visiwa vyetu kuna Nzi tofauti waharibifu wa Matunda wenye asili ya Afrika na Yule wavamizi kutoka Bara la Asia, wale wenye asili ya Afrika mashambulizi yao ni madogo kutokana na uwezo wao mdogo wa kuzaliana vile vile kuwepo kwa maadui zao, na walikua wakisababisha hasara kati ya asilimia 20% na 30%. Nzi Mvamizi mwenye Asili ya Bara la Asia anasababisha hasara kubwa hadi asilimia 90% kutokana kuzaliana kwa wingi, na kula aina nyingi za Matunda pia kutokua na madui kwa kua yeye ni mgeni katika Bara letu. Kwa sasa Nzi mvamizi amesambaa katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba hali iliopelekea wadudu wenye asili ya bara la Afrika kuonekana katika maeneo machache na kwa idadi ndogo sana. Leo tunamzungumzia Nzi mvamizi (Bactocera Invadens ) Jinsi ya muonekano wake, Uzazi wake, Athari zake  na Jinsi ya kumzibiti.

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>