
AFISA MKUU DIVISHENI YA UTUMISHI AMBAE PIA NI MSIMAMIZI WA MAFUNZO YA KILIMO CHA MINAZI, MBOGA NA MATUNDA NDGU. MASOUD SALUM ABDI AMESEMA SERIKALI YA WATU WA CHINA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUPITIA WIZARA YA KILIMO IMEANDAA MAFUNZO KWA WATAALAMU WA KILIMO ILI KUWEZA KUIMARISHA KILIMO NA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA KIBIASHARA NCHINI.Posted: 2024-12-13
Afisa Mkuu Divisheni ya Utumishi ambae pia ni msimamizi wa Mafunzo ya Kilimo cha Minazi, mboga na Matunda Ndgu. Masoud Salum Abdi amesema Serikali ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya kilimo imeandaa Mafunzo kwa Wataalamu wa Kilimo ili kuweza kuimarisha kilimo na kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Kibiashara nchini.
Masoud ameyasema hayo huko Shakani Wilaya ya Magharibi B Unguja wakati wa kutembelea Shamba la Uzalishaji wa Mazao ya kilimo cha Mboga ikiwa ni Miongoni mwa ziara za Kimasomo zinazotolewa na Wataalamu wa Kilimo kutoka nchini China.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa Wataalamu wa Kilimo ili kuongeza Uzalishaji wa mazao yenye tija nchini Sambamba na Kuzuia Wadudu waharibifu wa Mazao wasiweze kuathiri Mazao hayo hususan Minazi, mboga na Matunda.
Aidha Amewasisitiza Wataalamu hao kuzingatia vyema Mafunzo wanayopewa na Wataalamu ili Jamii iweze kujiekeza katika kilimo kwa vile kilimo ni mhimili wa Uchumi wa Kuchangia pato la Mkulima na pia ni tegemeo la mapato ya fedha ya ndani ya nchi.
Hata hivyo ameeleza kuwa Zanzibar inategemea zaid kilimo cha Mazao Mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mpunga, Viazi, Mihogo na ndizi ambapo Wakulima walio wengi wanajipatia kipato na Kupunguza Umaskini.
Naye Mtaalamu kutoka China Dr Yang Yang amesema Kutokana na Mashirikiano yaliyopo Wameona ipo haja ya kuja kutoa Elimu kwa Wataalamu wa Kilimo ili waweze kuimarisha kilimo na kuweza kutoa njia imara za Kupunguza Wadudu waharibifu wa Mazao.
Kwa Upande wao Washiriki wa Mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya Watu wa China kwa kuwapatia Mafunzo waliyopewa ambayo yataenda kuwasaidia katika kuwafundisha Wakulima njia mbadala ya kutumia dawa kwa ajili ya kudhibiti Wadudu waharibifu.
Mafunzo hayo ya Siku 21 yamefanyika kuanzia tarehe 25/11/2024 ambapo yamedhaminiwa na Serikali ya watu wa China kwa Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yamegharimu shilingi 126,900,000 kwa ajili ya Uratibu katika kufanikisha Mafunzo hayo Sambamba na Uimarishaji wa Mazao pamoja na Udhibiti wa Wadudu waharibifu.