
WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MHE: SHAMATA SHAAME KHAMIS AMESEMA WIZARA IMEKUWA IKIFANYA UTAFUTI WA MARA KWA MARA KWA KUJUWA TATHNINI YA WANYAMA PORI KATIKA MAENEO TOFAUTI YA HIFADHI ZA MISITU NA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA HIFADHI HIZO ZIILIOPO HAPA NCHINI.Posted: 2024-12-05
Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mhe: Shamata Shaame Khamis amesema kuwa Wizara imekuwa ikifanya utafuti wa mara kwa mara wa kiutaalamu kwa kujuwa tathnini mbali mbali ya wanyama pori katika maeneo tofauti ya hifadhi za misitu na kushirikiana na wadau wa hifadhi hizo ziiliopo hapa nchini.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa akijibu suala namba kumi na nane katika mkutano wa kumi na saba kikao cha sita kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi lililopo Chukwani Wilaya ya Magharib Unguja.
Mhe: Waziri amesema kuwa katika tafiti hizo hazijathibitisha idadai ya aina gani ya wangama pori wametoweka kwa ajili ya na imani ya ushirikina na kusisitiza kwamba usimamizi wa wanyama hao unafanywa kwa utaalamu wa kisayansi ambapo taaluma hiyo haikubaliani na matokeo hayo na imekuwa vigumu kuthibitisha kuwa wanyama pori wametoweka kwa njia hiyo.
Mhe. Shamata amesema utaalamu huo wa kisayansi umebaini kuwa kupunguwa kwa wanyama pori kumesababiswa na changamoto zilizojitokeza za ukataji wa miti, uharibifu wa misitu, uwindaji haramu wa wanyama, majanga ya moto yanayotokea na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani kote
Aidha Mhe: Waziri wa Kilimo amesema kuwa kwa mujibu wa utaalamu wa utafiti wa kisayansi ambao unatoa maamuzi ya majibu yaliyothibitishwa kuwa hakuna wanyama pori waliotoweka kwa njia ya kishirikina ndani ya misitu iliopo hapa Zanzibar.>
Hata hivyo Mhe: Shamata amesema kuwa Serekali inapinga vikali kuhusiana na masuala mazima juu ya ukatili wanaofanyiwa wanyama na Serikali Haitosita kumchukulia hatua za kisheria kwa yeyote atakae bainika kutumia wanyama kwa njia ya kishirikina
Mhe: Waziri wa Kilimo ameongezea kwa kusema Serekali imeweka Sheria ya wanyama na mikakati ya kuwalinda wanyama na bado inaendelea kuifata Sheria ya kitaifa na kimataifa na kuendeleza Sheria za nchi juu ya ustawi wa wanyama pori.