MKURUGENZI DARA YA MAENDELEO YA MIFUGO ZANZIBAR NDUGU. ASHA ZAHARAN MOHD AMEISISITIZA JAMII JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA MADAWA YANAYOSABABISHA USUGU WA VIMELEA VYA MARADH.Posted: 2024-11-26
Mkurugenzi dara ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar Ndugu. Asha Zaharan Mohd ameisisitiza jamii kufuata ushauri wa wataalamu juu ya matumizi sahihi ya madawa yanayosababisha usugu wa vimelea vya maradhi.
Ameyasema hayo alipofanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbni wa idara ya maendeleo ya mifugo maruhubi kufuatia wiki ya maazimisho ya uelewa usugu wa vimelea vya vinavyosababisha maradhi
Amesema ni vyema kusimamia utumiaji sahihi wa dawa hususani antibiotiki kwa kuhakikisha zinafuatwa njia sahihi za matumizi ya dawa kwa mimea ,wanyama na binaadamu ambayo hutumika kwa kutibu baktiria fangas na virusi ambavyo hubadilika na kuwa sugu na kuchelewa kupona.
Aidha amesema takriban vifo milioni 5 huripotiwa Kila mwaka Dunia vinavyosababishwa na usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya matumizi mabaya ya madawa ya mifugo na wanaadamu hivyo ni vyema kufuata miongozo inayotolewa na wataalum wa afya.
Hata hivyo amesissitiza kutolewa elimu zaidi utakao lenga athari za matumizi mabaya ya madawa kwa afya jumuishi ilikukabiliana na athari zinazoendelea kujitokeza na kuhakikisha kwamba binaadamu ,wanyama, mimea na mazingira ipo salama na endelevu.
Maazimisho ya wiki ya usugu wa vimelea huanimishwa Kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 November ya Kila mwaka kwa kutoa elimu kwa jamii.