
KAIMU MKURUGENZI MIPANGO SERE NA UTAFITI AMINA OMAR SALEH AMESEMA USHIRIKIANO WA SERIKALI YA WATU CHINA NA ZANZIBAR UNALETA MAFANIKIO KATIKA KUENDELEZA KILIMO NCHINI.Posted: 2024-11-25
Kaimu Mkurugenzi Mipango Sere na Utafiti Amina Omar Saleh amesema Ushirikiano wa Serikali ya watu China na Zanzibar unaleta mafanikio katika kuendeleza kilimo nchini.
Ameyaeleza hayo katika Chuo cha Utalii Maruhubi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya uimarishaji wa minazi na udhibiti wa wadudu wa matunda, mboga na viungo uliowashirikisha wakulima 50 kutoka Unguja na Pemba.
Amesema Wizara ya Kilimo,Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo ina lengo la kuwapatia mafunzo ya muda mfupi wakulima na wataalamu wa kilimo ambayo itawawezesha kufanya tafiti na kuendeleza kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Nae Afisa Mkuu Utumishi kutoka Wizara ya Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Ndugu. Masoud Salum Abdi amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili kwa lengo la kuelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya technolojia ya udhibiti ya wadudu waharibifu katika mazao ili kuinuka kiuchumi nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Ndugu. Amina Omar Saleh amesema Ushirikiano wa Serikali ya watu wa China na Zanzibar unaleta mafanikio katika kuendeleza kilimo nchini.
Ameyaeleza hayo katika Chuo cha Utalii Maruhubi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya uimarishaji wa minazi na udhibiti wa wadudu wa matunda, mboga na viungo uliowashirikisha wakulima 50 kutoka Unguja na Pemba.
Amesema wizara ya kilimo,Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo inalengo la kuwapatia mafunzo ya muda mfupi wakulima na wataalamu wa kilimo ambayo yanawawezesha kufanya tafiti na kuendeleza tafiti za mazao ambayo yataleta Mafanikio.
Nae Afisa mafunzo Masoud Salum Abdi amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili lengo ya kuwaelimisha wakulimajuu ya matumizi ya teknolojia ya kisasana kuweza kudhibiti wadudu haribigu wa mazao ya mazao ya matunda mboga mboga na viungo Amesema mafunzo hayo ni ya mara ya pili kwa kufanyika kwa Zanzibar ambayo yameleta manufaa kwa wakulima na kwa kuweza kubadilishana taaluma kutoka kwa wataalamu wa China na kubadilishana mawazo na wakulima kwa njia ya vitendo.
Nae mtaalam Mr Counselor Wung Yu kutoka serikali ya China amesema Serikali ya China Iko tayari kuunga mkono wakulima wa Zanzibar kwa kuwapa taaluma itakayowaletea mabadiliko ya kiuzalishaji na kuweza kupambana n wadudu wa mazao.