
WAKULIMA WAMETAKIWA KUTUMIA MBEGU BORA ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA NCHINI.Posted: 2024-11-14
Wakulima wametakiwa kutumia mbegu bora ili kuongeza uzalishaji wa Mpunga nchini.
hayo yamesemwa na Afisa ufuatiliaji na tathimini Hidaya Ali Abdallah kutoka wizara ya kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo
alipokuwa akifungua mafunzo kwa wakulima wazalishaji mbegu za Mpunga katika ofisi za kilimo Maruhubi iliyowashirikisha wakulima wa mpunga kutoka Mabonde mbali mbali ya Unguja .
Amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwapa elimu wakulima juu ya uzalishaji mbegu kwa njia za kitaalamu ili kuendeleza mbegu asili zenye sifa za kukuza uzalishaji na kutoa mavuno yatakayo saidia kufikia kujitosheleza na kuwa na uhakika wa chakula.
Aidha amesema utekelezaji wa mradi huo utajikita katika kuboresha miundombinu ya Umwagiliaji, ujenzi wa vituo vya wakulima na Maghala ya kuhifadhia mbegu ambavyo vitagharimu shilingi za kitanzania Milioni 15.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mbegu kutoka katika Mradi himilivu wa mifumo ya chakula Tanzania Mohamed Faida Haji Amesema wakati umefika kwa wakulima kuhakikisha wanazalisha mbegu za mpunga katika kiwango kinachotakiwa
Amesema Suala la kurejesha mbegu za Mpunga mara kwa mara hupelekea kuzalishwa kwa wadudu na Maradhi na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa wa zao la Mpunga hivyo ipo haja kwa wakulima kuyatumia mafunzo hayo ili kuwaletea mabadiliko ya kiuzalishaji .
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema wamefaidika kupitia mafunzo hayo na watakuwa wawakilishi bora wa wenziwao pia kushirikiana ipasavyo na kufuata maelekezo vizuri waliopatiwa na wataalamu