
WAZIRI WA KILIMO, UMWAGILUAJI, MALIASILI NA MIFUGO MHE: SHAMATA SHAAME KHAMIS AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IKIWEMO NA TAASISI ZAKE ITAENDELEA KUFANYA JITIHADA KATIKA KUSIMAMIA SUALA LA UPANDAJI WA MITI NA UTUNZAJI WA MITI ASILI KATIKA MAENEO MBALI MBALI NCHINI. Posted: 2024-11-08
Waziri wa kilimo, umwagiluaji, maliasili na mifugo mhe: shamata shaame khamis amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar ikiwemo na taasisi zake itaendelea kufanya jitihada katika kusimamia suala la upandaji wa miti na utunzaji wa miti asili katika maeneo mbali mbali nchini.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na wadau washauri wa kutunza miti asili na kupunguza hewa ukaa huko katika ukumbi wa kilimotija Maungani Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Amesema ni Muhimu kupanda miti mingi ya asili na miti ya kivuli hususan katika manispaa ya Mji Mkongwe ambapo hali hiyo itasaidia kuweka mandhari nzuri na yenye haiba ya kuvutia na kupelekea kupatikana hewa safi na kupunguza hewa ukaa Zanzibar.
Hata hivyo Mhe: Shamata amesema kuwepo kwa miti mingi Zanzibar kutasaidia kupunguza hewa Ukaa chanzo cha mvua upatikanaji wa dawa za asili, chakula cha wanyama na binaadamu pamoja na mazalia ya wanyama na shughuli za utalii.
Nae Mhadhir Mwandamizi Mshauri wa Mradi wa kutunza Miti asili na kupunguza hewa Ukaa kutoka Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dr Abdalla Ibrahim Ali amefahamisha kuwa pamoja na ujenzi unaoendelea wa kujenga barabara kumekuwa na ongezeko kubwa la ukataji wa miti kiholela jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa ya uharibifu wa hali ya hewa nchini.
Aidha alisema Zanzibar ina hadhina kubwa ya miti asilia ikiwemo miti ya dawa ambapo kwa sasa miti hiyo imepotea na miti mengine iliyokuwepo katika maeneo ya Mji Mkongwe ya Manispaa ya Mji wa unguja na Pemba.
Wakati huo huo Mhe Shamata alipata fursa ya kuzungumza na Wafadhili kutoka Ujerumani katika Manispaa ya Jiji la Potsdam ukiongozwa na Meya wa Jiji la Manispaa ya Zanzibar.