
KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO AMESEMA SEREKALI IPO TAYARI KUSIMAMIA UMOJA WA WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI MBEGU ILI KUPATA MBEGU MORA ZENYE TIJA KWA WAKULIMAPosted: 2024-04-24
Katibu Mkuu Wizara ya kilimo, Umwangiliaji, Malisili na Mifugo Ali khamis Juma amesema Serikali ipo tayari kusimamia Umoja wa Wazalishaji na wasambazaji Mbegu ili kuweza kuwa na mbegu zenye Ubora zitakazo leta manufaa kwa Wakulima.
aliyasema hayo katika hotel ya Maru Maru Forodhani Unguja wakati akifunguwa Warsha ya Wadau wa Uzalishaji Mbegu iliyowashirikisha wataalamu watafiti, Tasisi binafsi za kilimo,wakulima na Makapuni ya usambazaji wa Mbegu kutoka Zanzibar na Tanzania Bara
Amesema Mbegu bora kwenye Kilimo ndio msingi wa mafanikio ya uzalishaji wa Mazao hivyo kuwepo kwa mashirikiano na Wazalishaji na wasambazaji wa biashara ya Mbegu, kutaisaidia Serikali kujua matatizo na mafanikio katika uzalishaji wa mbegu za Mboga Mboga ,matunda na nafaka.
Aidha alieleza kuwa Zanzibar ina eneo dogo la uzalishaji wa Mazao hivyo uzalishaji wa mbegu na watafiti ni muhimu uzingatiye Mbegu zitakazo weza kustahamili ukame,maradhi na miongo tuliyonayo.
Nae Meneja wa Mradi wa usimamizi wa Taasisi ya World Vegetable Center Tanzania Jeremiah Sigallah amesema Lengo la Warsha hiyo ni kupata mawazo kwa wadau na kuweza kutengeneza Umoja utakao weza kutoa tarifa za haraka kwa wazalishaji mbegu na makampuni yanayo sambaza mbegu duniani na kuweza kupata mbegu bora chotara na za asili na kuendeleza biashara ya Mbegu kukuwa zaidi na kuwapatia tija wakulima.
Wakitoa Maoni yao washiriki wa warsha hiyo waishukuru taasisi ya World Vegetable centre kwa kuwapatia mafunzo hayo yatakayo wajengaya uwelewa wa mifumo ya mashirikiano ya biashara ya uzalishaji mbegu duniani.
Warsha hiyo ya siku moja imefadhiliwa na shirika la maendeleo la watu wa Marekani USAID na World Vegetable centre.