
KATIBU MKUU AWAHIMIZA WAKULIMA KUTUNZA MICHE NA VIFAA VYA ZAO LA KARAFUU Posted: 2024-04-15
Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Ali Juma Khamis amewataka Wakulima wa Mikarafuu kutunza miche na Vifaa wanavyopewa ili lengo la kukuza Uzalishaji wa Zao hilo liweze kufikiwa.
Hayo ameyasema huko Ofisini kwake Maruhubi Wakati wa Makabidhiano ya Vifaa vya Uzalishaji Miche ya Mikarafuu.
Amesema Lengo la Utoaji wa vifaa hivyo ni kutokana na Mashirikiano yaliopo na ZSTC katika kuwasaidia Wakulima wa Zao hilo katika kuthamini Mchango wa Sekta ya karafuu hasa katika eneo la Ukulima wa karafuu.
Aidha Katibu huyo ametoa wito kwa Wananchi watakaokabidhiwa vifaa hvyo wajitahidi kuitunza mikarafuu hiyo ili iweze kuzaa na tija iweze kupatikana.
Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la biashara ZSTC Soud Said Ali amesema karafuu ni Miongoni mwa vyanzo vikubwa vya Mapato ya fedha za nje Ukiachia Utalii, hivyo anaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuwapa Mashirikiano na kuzidi kupiga hatua ya Maendeleo nchini.
Kila mwaka Shirika la Biashara ZSTC hutoa vifaa vya miche ya mikarafuu ambapo kwa mwaka huu wametoa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni nane laki tisa na arobaini kwa Upande wa Pemba na kwa Upande wa Unguja ni shilingi milioni tano laki nane na hamsini.