SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEA KUIMARISHA MASHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KUKUZA KILIMO BORA ZANZIBARPosted: 2024-04-09
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha Mashirikiano na Mashirika ya Maendeleo na Binafsi katika kuongeza Uwezekezaji ambao utasaidia kuwa na kilimo endelevu na Chenye tija.
Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis ameeleza hayo wakati alipofungua Kikao cha Mkakati wa Majumuisho ya Uwezekezaji katika mazao ya Maziwa na Mwani huko katika Ukumbi wa ZURA.
Shamata alisema fursa za Uwekezaji zilizomo katika Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Maziwa pamoja na Mwani ambayo yana Mchango Mkubwa katika kuinua kipato cha Wananchi wa Zanzibar na Kukuza Uchumi.
"Leo tumehudhuria hapa katika kujadili shughuli za Mnyororo wa Thamani kwa Mazao pamoja na Mwani ambapo kikao hichi kitastawisha shughuli hizi katika maono ya kukuza Uwezekezaji na Uchumi wa kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa" aliongea Shamata
Hata hivyo Mhe. Shamata alisema Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar 2021 hadi 2026 umebeba Taaswira sahihi ya kuinua sekta ya kilimo chenye tija kwa kuongeza Uzalishaji, tija, Usafirishaji wa Mazao nje ya nchi pamoja na kuongeza mapato yatokanayo na Uongezaji wa Thamani kwa bidhaa za kilimo, Uzalishaji wa Vyakula kupitia kilimo hai na kuimarisha Utalii wa kimazingira kwa Kuhifadhi Uoto wa Asili na Viumbe Hai wa kipekee nchini.
Nae Msaidizi wa Mwakilishi wa Fao nchini Tanzania na Mkuu wa Mradi Charles Tulahi alisema Mpango wa Hand in hand initiative ni wa kipekee ambao unazingatia matumizi ya taarifa sahihi katika kuondoa Vikwazo vya Maendeleo ya Sekta ya kilimo
"Matumizi haya Sahihi ya Takwimu na taarifa za kilimo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali, wafadhili wa Sekta binafsi ili kufahamu Uwekezaji na Sera sahihi zenye tija katika Sekta hii." alieleza Charles
Sambamba na hayo Charles aliendelea kwa kusema kwa kuzingatia Ombi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar FAO imekua tayari kupanua wigo wa Utekelezaji wa Mkakati katika kulenga sekta ya Uvuvi na Mifugo hadi Visiwani Zanzibar ambapo upanuzi huo ni muendelezo wa Utekelezaji kwa Mkakati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mnyororo wa Thamani wa Zao la mwani na Maziwa.
"Tumeona kua kuna umuhimu mkubwa wa Zao la Mwani kwani Utafiti wa Repoa unaonesha kuwa Wakulima wa mwani wengi wao hasa ni wanawake ambao wanapata Kipato kidogo na kisichoridhisha" alisema msaidizi huyo.
Mapema akizungumza katibu Mkuu kutoka Wizara ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Hamad Bakar Hamad alisema Wajasiriamali ambao wamo katika Mnyororo wa Thamani wanatakiwa kupatiwa Uwezo wa Zao la mwani na Maziwa kwani takwimu zinaonesha kwamba Mwani umeajiri watu wengi wasiopungua 16 elf zaid ya asilimia 50 hadi 60 ambapo mpango wa Hand in hand ukitekelezwa Zanzibar unaweza kuwapa nguvu wanawake na kuwavutia Vijana kuingia katika Mnyororo wa Thamani wa Mwani na Maziwa.
Kwa Upande wa Mfugaji wa Ngombe wa Maziwa Mohd Pongwa Mohd kutoka Chuini alieleza kuwa Ukosefu wa Masoko unapelekea Wafugaji wa Ngombe wa Maziwa kuwa na hali duni pamoja na kuwa na eneo dogo la ardhi hivyo anaiomba Serikali iwasaidie katika kuwapatia maeneo ya Uzalishaji sambamba na kupatiwa taaluma ikiwemo na pembejeo.
Mkutano huo wa siku moja Umehudhuriwa na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Maafisa waandamizi, Sekta binafsi pamoja na Wazalishaji wa kilimo