
MHE. JUMA ALI KHATIB AMEISHAURI TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO (ZARI) KUANDAA MPANGO WA MAKADIRIO YA UZALISHAJI WA MAZAO NA MICHEPosted: 2023-08-23
Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za Serekali ya Baraza la Wakilishi Mhe. Juma Ali khatib ameishauri Taasisi ya Utafiti wa kilimo (ZARI) kuandaa Mpango wa makadirio ya uzalishaji wa mazao na miche katika msimu mkubwa na mdogo na kuweza kujua mapato na mahitaji yatakayowezesha kuongeza uzalishaji.
Hayo aliyasema Kizimbani wakati wa kikao cha kupitia hoja za Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, kilichowashirikisha viongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar - ZARI, Amesema Tasisi inawajibu wa kuwa na muongozo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mauzo ya mazao, miche na utalii na pia kuwa na mpango wa uzalishaji wa kuendeleza tafiti za kilimo.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Ndugu. Seif Shaaban Mwinyi ameiomba Serikali kuwa na mipango na tathimini itakayoendana na kima cha fedha watakachoweza kufikia sambamba na kuwezeshwa kubakishiwa fedha ili waweze kuendeleza uzalishaji wa miche katika kituo hicho.