
WAZIRI MHAGAMA ASEMA MAONESHO YA KILIMO NI NJIA PEKEE YA WAKULIMA KUPATA KUJIFUNZA MBINU BORA NA MATUMIZI YA ZANA ZA KISASAPosted: 2023-08-11
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Jenestar Jowakim Muhagama Amesema maonesho ya kilimo ni njia pekee ya wakulima kupata kujifuza mbinu bora za ukulima wa kitaalum na matumizi ya zana za kisasa na kuwaletea mafanikio katika uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini. Aliyasema hayo Dole Kizimbani wakati akifunga Maonesho ya wakulima nane nane yaliyowashirikisha wadau 275 wakiwemo wakulima, wajasiriamali, Tasisi binafsi na Tasisi za Serikali.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Mhe Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi inafanya juhudi kubwa, kuibadilisha nchi kuweza kuleta madiliko katika sekta za uzalishaji wa chakula na kukidhi mahitaji ya wananchi. Amesema Zanzibar imepiga hatua nzuri na matokeo ya maonesho yatawezesha wakulima kujifunza vitu vipya na kupelekea kuleta mapindizi ya kilimo ambapo wataźalisha kwa wingi mazao ya biashara ambayo yataongeza mnyororo wa thamani wa mazao na kuuza ndani na nje ya nchi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo amesema maonesho hayo yana lengo la kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima yamedumu kwa siku 10 na kugharimu jumla ya Shilingi Milioni Mia Tano fedha za kitanzania.
Akitoa Maelezo kwenye ufungaji huo Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe shamata Shaame khamis ameishukru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mashirikiano yao na kuyawezesha maonesho ya kilimo kwa mwaka 2023 kufanikiwa. Aidha aliwashukru wadau na wananchi wote waliochangia na kuwaomba wakulima kuzidisha bidii na kuja na mbinu mpya za kilimo katika maonesho yajayo.