MKOA WA KUSINI UNGUJA WAPANDA MITI KATIKA MSITU WA HIFADHI WA JAMBIANI MUYUNIPosted: 2023-05-11
Jumla ya miti asili elfu mbili imepandwa katika eneo la hifadhi ya jambiani muyuni katika eneo lililoathirika na moto lenye ukubwa wa takribani hekta mia moja ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Rajab Yussuf Mkasaba Afisa misitu wa wilaya hiyo Idrisa Hamdani idrissa amesema hatua hiyo itasaidia kurejesha uhalisia uliopotea katika eneo hilo.
Amesema msitu wa hifadhi ya jambiani unafaida kubwa hivyo amewataka wakulima kuacha kutumia moto wakati wanapo andaa mashamba yao ili kupunguza athari zinazoweza kuepukika.
Mkuu wa kituo cha Jozani Aziza Yunus Mchimbi amewataka wakulima kutumia njia mbadala wakati wanapofanya shughuli za kilimo ili kutunza mazingira yaliyopo ndani ya hifadhi hiyo na kuwasisitiza kuepukana na uharibifu ambao ni hatari kwa uhai wa misitu.
Nao wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti wamesema watahalikisha wanaitunza miiti hiyo kwa kushirikiana na mamalaka husika ili lengo liweze kufikiwa .
Upandaji wa miti umewashirikisha wananchi wa shehia zilizozunguka hifadhi,Idara ya misitu na taasisi ya Jane Goodall institute Roots and Shoots inayosimamia uhifadhi wa msitu wa jambiani Muyuni.