
WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI MICHE YA MIKARAFUUPosted: 2023-03-15
Waziri wa Kilimo, Umwagilaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis akiwa katika uzinduzi wa ugawaji wa miche ya mikarafu kwa msimu huu alisema karafuu ni zao linaloimarisha uchumi wa zanzibar kwa kuwa ni zao la biashara linalo vitangaza viziwa vya unguja na pemba duniani kote pamoja na kuingizia serekali mapato.
Amesema Serekali kwa kutambua na kuona thamani ya zao la karafuu inaendelea kufanya juhudi za kupandisha bei ya karafuu,kuwapa vifaa na mikopo pamoja na kuzalisha kwa wingi miche ya mikarafuu na kuitoa bure kwa wakulima ili wakulima waweze kuliendeleza zao hili kwa manufaa ya nchi yetu Aidha Mhe. Shamata amewataka wakulima wa takao pewa miche hiyo kuipata na kuishughulikia ili iweze kukuza uzalishaji na kuahidi kusimamia vitalu vilivyopo katika mikoa na wilaya za unguja na Pemba. .
Mhe Waziri amewasisitiza wakulima kutoipoteza miche ya karafuu kwani kutaitia hasara serekali ambayo inataka kuona jitihada za upandaji wa miche ya mikarafuu zinaleta manufaa kwa kuzalisha ziada ya karafuu itakayo ijengea sifa na kuresha hadhi ya uwasili wa zao la karafuu na kukuza uchumi wa nchi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mhe Ayuob Mohamed Mahmoud amesema karafuu ni zao la Taifa kwa kuliona hilo Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Hussen Ali Mwinyi ameridhia kupewa wakulima miche ya mikarafuu bure hivyo wakulima waitumiye fursa kufanya jitihada ya kuifatilia na kuipanda kitaalamu na kuweza kulifikia lengo la Serekali