
KATIBU MKUU AKABITHI TANI 88 ZA MBEGU YA MPUNGAPosted: 2023-02-27
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwangiliaji, Maliasili na Mifugo Ndg: Seif Shaaban Mwinyi amekabidhi tani 88 za mbegu za mpunga aina ya Saro 5, TXD 88 na SuPa PADDY yenye gharama ya shiling za kitanzania 227,000,000 kwa jumuiya ya wa wakulima wa bonde la Cheju ambayo itauzwa kwa wakulima kwa bei ya shiling 1300 kwa kilo moja. Amesema hayo huko chenju alipokuwa akikabidhi mbegu hiyo kwa Jumuiya ya Wakulima ya bonde la Cheju
Amesema fedha za ununuzi wa mbegu hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi kwa lengo la kuwasaidia wakulima wa mpunga kupunguza changamoto za mbembejeo zinazo wakabili ikiwemo mbegu bora. Aidha ameeleza kuwa mbegu hizo aina ya SARO 5, TXD 88 na SUPA PADDY ambazo zimenunuliwa katika taasisi ya ASA ya Morogoro zitatumika kwa wakulima wa Unguja na Pemba ambapo zitauzwa kwa bei ya ruzuku ya shiling 1300 kwa kilo moja Hata hivyo amesema serekali ipo katika mazungumzo na Tanzania bara ili kuweza kusawazisha suala la mbolea kwa vile malamiko ya wakulima wa mpunga ni kuwa bei ya mbole ni kubwa inayoletwa na wafanyabiashara
Nae Mwenyekiti wa jumuiya ya wakulima wa mpunga bonde la cheju Omar Idd Ame amemshukru Rais kwa msaada na kusema mbolea hiyo imekuja kwa wakati kwani wasingeweza kuwahi msimu wa kilimo cha mpunga kwa mwaka huu kwakuwa hawakuwa na mbegu walizoweka wakulima na kuahidi kuzitumia mbegu hizo kwa kuzidisha juhudi katika uzalishaji wa mpunga