
SEKTA YA UTALII ITAIMARIKA IKIWA WAGENI WATAKUWA NA IMANI KUWA ZANZIBAR WATAPATA CHAKULA SALAMA AMBACHO HAKINA MADHARAPosted: 2023-01-06
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uwezeshaji, Wananchi Kiuchumi Mhe: Mudrik Ramadhani Soraga amesema Sekta ya utalii itaimarika ikiwa wageni watakuwa na Imani kuwa Zanzibar watapata chakula salama ambacho hakina madhara. Alisema serikali kwa kutambua suala hilo imeimarisha miundonbinu ya kuhifadhia chakula kwa kulinda usalama wa wageni Kuimarisha sekta ya utalii nchini
Alisema suala la kudhibiti Sumu kuvu ni muhimu ndio maana serikali kupitia Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo imeamua kujenga maghala ya kuhifadhia chakula kulinda usalama wa chakula kwa watumiaji. Alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kulitumia ghala hilo kuhifadhia mazao yao kuepusha kuharibika na kutokuwa salama kwa mlaji. Aidha aliwataka wataalamu wa Kilimo kulitunza ghala hilo ili litumike kwa muda mrefu Alisema hayo Kizimbani Wilaya ya Magharib “A” mara baada ya ufunguzi wa ghala la kuhifadhia chakula ili kudhibiti Sumukuvu ikiwa ni shamra shamra za kuelekea miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwàka 1964.
Nae, Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na mifugo Shamata Shaame Khamis alisema Serikali inajali maisha ya wananchi ndio maana ikaamua kujenga ghala kuwapa nafasi wananchi kwenda kuhufadhi mazao yao Alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuacha kulima maeneo ya kilimo ambayo yametengwa kwa kilimo kuongeza uzalishaji wa chakula. Aliwataka wananchi kulitumia ghala hilo kuhifadhi mazao yao kuondosha usumbufu wa kuharibika na kuepusha kuwa na Sumukuvu. Aliwataka wakulima kulima kwa kufuata maelekezo ya wataalamu kuongeza teknolojia na utaalamu wa kisasa kwenye kilimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Nd: Seif Shaabani Mwinyi alisema ghala hilo litagharimu milioni 930.5 hadi kukamilika kwa mradi na utakuwa na uwezo wa kuchukua tani 1500 za mazao. Alisema ujenzi wa ghala hilo kitaondosha kutokea kwa sumu kuvu ambayo ni hatari kwa afya za binaadamu na kuwa katika ubora na kuwa na viwango vinavyoshauriwa na wataalamu. Alisema ujenzi wa ghala hilo ulianza mwaka 2021 na utamalizika 2024 na unaeneo la kukaushia mazao, Ofisi, vyoo na Tangi la kuhifadhia maji ya mvua.
Mkuu wa Wilaya ya Magharib “A” Suzan Peter Nkunambi alisema mradi huo ni muhimu kwa Maendeleo ya wananchi ambao umelenga kudhibiti Sumukuvu. Aliitaka Wizara chakula kitakachotoka katika maeneo hayo sambamba na kuzitaka Wizara kuyadhibiti maeneo ya ki limo ili wananchi waendelee kulima na kuongeza chakula kuondokana na upungufu wa chakula.