
MAKAMO WA KWANZA WA RAIS MH. OTHMAN MASOUD OTHMAN AMESEMA KILA MMOJA ANAWAJIBU WA KULINDA NA KUTUNZA HIFADHI HAI YA JOZANI GHUBA YA CHWAKAPosted: 2023-01-04
Makamo wa Kwanza Wa Rais Mh. Othman Masoud Othman amesema kila mmoja anawajibu wa kulinda na kutunza hifadhi hai ya jozani ghuba ya chwaka ili kusaidia kubaki salama na kuwa kivutio kikubwa cha wageni Akizindua hifadhi hiyo huko jozani wilaya ya kati Mh Masoud amesema hatua hiyo itasaidia hifadhi hiyo kutoathiriwa na wananchi ambao hawana uwelewa kuhusu hifadhi hai
Amesema kumekua na matatizo mengi katika hifadhi hai kwani wapo watu hutumia hifadhi hiyo kwa kukata miti, kuchoma misitu, kuwinda wanyama na kuleta athari ndani ya msitu huo . Aidha amesema ili hifadhi hiyo iendelee kubaki salama ni lazima kila mmoja awe mlinzi wa mwenziwe katika kulinda hifadhi hiyo ili kulinda rasilimali zilizopo kubaki salama.
Amefahamisha kua hifadhi hiyo imepanda hadhi kutokana na vigezo vingi vilivyo kuwa nazo ikiwemo kuwa na biyoanuni za kutosha kama vile kima punju ushirikishwaji wa wanajamii na kuchangia maendeleo ya kiuchumi kwa kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake waziri wa kilimo umwagiliaji maliasili na mifugo Shamata Shaame Khamis amesema mwaka uliopita kumekuwa na Ongezeko kubwa la wageni wanao tembelea katika hifadhi hiyo ambapo kuna zaidi ya elfu hamsini na mbili walitembelea hifadhi hiyo na kusaidia serikali kupata mapato. Amesema serikali itaendelea kusimamia sheria na kanuni kwa vitendo ili kusaidia hifadhi hiyo kuwa endelevu.
Wakisoma risala fupi muakilishi wa jumuiya ya uhifadhi wa mazingira Awesu shaban Na mwenyekiti wa kamati ya taifa ya hifadhi hai ambae pia ni mkurugenzi mkuu wa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC Dkt Mena Hungwe Jangu wamesema licha ya hifadhi hiyo kuwa kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi hai lakini bado kumekua na changamoto nyingi ikiwemo uwelewa mdogo wa wananchi juu ya hifadhi hai, uchomaji misitu na kuleta athari kwa taifa.