
KATIBU MKUU APOKEA UJUMBE KUTOKA IFADPosted: 2022-07-18
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Ndugu Seif Shaaban Mwinyi amepokea ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la IFAD hapo Ofisini kwake Maruhubi Zanzibar na kuongoza kikao na kujadili mafanikio mbalimbali ya mashirikiano ikiwemo mradi wa kukabiliana na athari za uviko 19 katika sekta ya kilimo.
Ujumbe huo uliongozwa na Bi. Jacqueline Machangu Motcho ambae ni Country Officer East and Southem Africa-IFAD, Bi. Jacqueline alieleza juu ya malengo makuu ya mradi huo wa IFAD.